Unaweza
kumpeleka punda kunywa maji na wala asinywe hayo maji, unaweza kumtwanga
mpumbavu kwenye kinu na wala upumbavu wake usimwishe. Kuna habari ya ya mtu mmoja yeye alikuwa anataka kujua siri ya mafanikio. Alikwenda kumuona mtu mwenye busara,
“Akamuuliza nifanyeje ili niwe na mafanikio?”.
Mzee mwenye busara akajibu akasema; “ Unatakiwa ubadilishe kufikiria
kwako kisha ubadilishe matendo yako na
mwisho uwe tayari kufanya vitu fulani vitakavyokufanikisha” Yule mtu akatulia na kufikiria maneno ya mwenye busara na tena
akaondoka. Hakutaka kubadilisha
kufikiria kwake, akutaka kufanya hayo yote kwani aliona kuna mambo yake
yataharibika kwa kubadilisha yaliyo kwenye fikra zake, alikuwa mbishi
kubadilika na kwahiyo aliamua kushindwa.
Ndugu zangu waume kwa wanawake, ilikuwa ni wakati ule wa zamani. Je! wewe unafikiria nini, Ebu badilisha
kufikiria kwako na pia badilisha maisha yako kwa kuwa tayari kuthubutu na
kufanya kitu unachotaka kufanya kwa wakati!!!!
Tunafika
mahali tunafikiria. Kile unachokifikiria ndiyo kitakusababisha ufanye na malengo yako
yatakwenda badala yake. Wote
wanaofikiria kuhusu malengo yao ni wale
wanaofikia malengo, ila wale wote
wasiofikiria kitu nao hawawezi kufanya kitu.
Wote wasiokuwa na wazo wanaenda
kuwa na fikra zilizochangamana na hofu, wasiwasi na woga. Tangu walivyofikiria hivyo wanaenda kupata
hayo; wamejazwa na michanganyo vichwani mwao, hofu, wasiwasi na woga. Kama
unafikiria hauna kitu, lazima
hutakuwa hauna kitu; ukifikiria makubwa, lazima upate makubwa.
Na
Lusako Mwakiluma
No comments:
Post a Comment