Muda gani
inakuchukua kubadilisha maisha yako.
Watu wengi wanaamini kwamba ni muda mrefu sana sio kweli ni siku moja tu
ya kufanya maamuzi. Ni kweli masaa 24 tu
yanaweza kubadilisha maisha yako kabisa
kabisa. Kwanini inakuchukua muda mrefu
kufanya maamuzi? Imefika mahali unaamua
halafu unakata tamaa. Unajua ndege inapoanza kupaa huwa inachukua
kasi na ikishachukua kasi inaanza kutafuta usawa wa kuruka kwenda juu. Rafiki yangu ikishashika kasi hata kama
umesahau kitu rubani hawezi kusimama au kurudi na kuchukua ulichokiacha ni
safari mpaka ifike mwisho wa safari yake.
Ndivyo na
wewe unavyotakiwa kuwa kwamba, ukiamua sasa naanza safari ya mabadiliko ya
maisha yako hakuna kugeuka nyuma kumbuka Ruthu aligeuka nyuma akawa jiwe la
chumvi ina maana kama uliwahi kufanya biashara huko nyuma ukafilisika usigeuke
kukumbuka magumu ya ile biashara hii ni biashara mpya soma Isaya 43:18 katika
maandiko ya biblia takatifu -Nanukuu:Msiyakumbuke mambo ya kwanza wala msiyatafakari mambo ya
zamani. “In English don’t talk about the past, live today live fully”. Mtu anaweza kuwa na wazo la mabadiliko akakaa
nalo muda mrefu sana baadae lile wazo lake likafa kabisa na kupotea kwa sababu
hakuchukua maamuzi. “Ideas goes away
direction stays”. Kama muda wa
mabadiliko umefika lazima uchukue maamuzi thabiti na kuanza kwenda mbele bila
hofu yoyote.
Dr Howard
Thurman Theologia mkubwa ulimwenguni alisema kwenye hotuba zake “kwa wakati
kila dakika unayozalisha hofu ndio muda
unaoruhusu adui kushinda”.
Majaribu yanakuja lakini
unamruhusu adui kushinda” Muda unapoamua
kuchukua maamuzi sahihi na kwenda
mbele na maamuzi yako ni kwenda kubadilisha maisha yako” Adui hana nafasi akikuona una hofu wala
kuyumba anabaki anajiuliza kuna nguvu gani ndani yako? kumbuka pia wewe ni mfano wa Mungu iwe una
imani tofauti bado Mungu ni wa wote na
ana ukuu katika maisha yetu. Kuna
marafiki zangu Fortune na Glory wao walikuwa na semina, walivyoanza semina yao
walianza na swali “unakwendaje kufanikiwa katika maisha yako” wahudhuriaji
walibaki wakiguna na kuulizana bila majibu yoyote: Jim na Naomi walijibu swali na kusema ni “kuamua tu”
Umuhimu wa kubadilisha maisha yako ni suala la kuamua tu.
Og Mandino
aliiita “Siri ya kuamua” Les Brown aliita “ni hali ya kuamua” Anthony Robbins
aliita “mwisho wako unategemea na maamuzi yako”. Hivyo unataka uwe hivyo?
Umuhimu wewe ni nani na huko wapi? Na hapo ulipo upo kwa sababu ya kuamua
kushinda au kushindwa kufanya maamuzi.
Amua maisha yako kabla maisha hayajaamua badala yako. Tunatakiwa tuongoze maisha yetu kwa kufanya
maamuzi ya kuchagua jinsi gani tuishi. Maamuzi yako ndio siku utakayobadilisha
maisha yako “uamuzi ni ufunguo wa kubadilisha maisha yako” Hivyo fanya maamuzi leo
kwanza ili ujue wapi unatakiwa kwenda? Kwanza lazima uwe na mtazamo au ndoto!!!
No comments:
Post a Comment