Mimi
sidhani kama kuna nguvu yoyote ya mafanikio duniani, zaidi ya maneno
haya “ katika mafanikio duniani ni zaidi
ya kujidhatiti na kutokata tamaa”.
Maisha ya kutokana tamaa
yanashinda kila kizuizi cha hapa duniani, hata nguvu zozote za kiasili” Bwana John D. Rockfeller, alizaliwa mwaka
1839 – kufariki 1937; alikuta baba yake na ukoo wake ni wa kimaskini. Zaidi baba yake mwenyewe hakuwa na muda na mtoto wake, katika
kukaa kwake John alijitengenezea njia
zake mwenyewe kwa mfumo wake mwenyewe.
Hakusema eti… familia yetu ni maskini … oh ukoo wangu ni maskini. Alisimama yeye kama yeye na kufanya kazi kwa
bidii na alikuwa mwanamapinduzi wa viwanda duniani.
Na wewe
unapokutana na vikwazo katika maisha yako simama katika nafasi yako jitahidi
uvishinde ili uweze kwenda upande wa pili, kila kikwazo kina maana na ndio
maana kuna mitihani ambayo inatusababishia kuvuka daraja na kwenda mbele,
mitihani isingekuwepo tusingeweza kusoma shule.
Na majaribu yasingekuwepo watu wangeridhika na hali walizonazo. Mtu akipitia majaribu na changamoto anakuwa
mwalimu mzuri sana kwa mwingine. Kumbuka
kila tatizo unalopitia kuna mtu mwingine aliwahi kupitia kabla yako unatakiwa
uwe makini na kuweza kuwahoji watu jinsi ya kutatua matatizo unapoona kuna
ugumu wa aina ya tofauti.
Na ukiona
mambo ni rahisi wakati wote basi ujue haupigi hatua yoyote katika maisha yako
unakuwa mtu wa kuridhika siku zote. Wapo
watu wengi sana waliofanikiwa kuweka rekodi ya dunia, ambao ni mashujaa wakubwa wa dunia, na si kwamba walikuta maisha ni matamu kuyaishi ila waliamua
kuyatengeneza maisha yao kwa mifumo yao.
Akina Frederick Douglas, tena
ndugu huyu alisema maneno haya “Ukiamua
kuyakubali maisha ya kawaida kwa
kutumia uwezo wa kawaida hata kama
ukipata fursa ya maisha utajikuta
ukifanya kazi na kufanya kazi zote za miaka ya maisha yako yote
mpaka unakufa maskini”. Fanya
zaidi ya kawaida. Nenda zaidi ya
mazoea.
Nakubaliana
na kauli ya Rais Mweusi wa kwanza wa Marekani, Barack Obama aliyesema maneno
haya “Kutengeneza alama yako duniani ni kazi, lazima ulipie gharama”. Lazima
upambane, lazima upigane bila
kuvunjika moyo. Kama ingekuwa rahisi
kila binadamu angefanya lakini inawezekana kwa kila binadamu yeyote atakayeamua
kujidhatiti na kuvumilia kwani ukiwa njiani kuyafikia haya utasukumwa na
vizuizi vya kila aina na hata kuanguka mara kadhaa. Jambo la muhimu ni kuingia na kuyafanya
uyatakayo duniani na si kukimbia kuangushwa njiani, kubali kujifunza na kukomazwa na magumu unayoyapitia kwa
kuchukua hatua katika kila muda unapoangushwa au unaweza kujiaibisha mwenyewe kwa kutochukua hatua na kurudi nyuma baada ya kuangushwa au
ukaamua kupigana na kupigana mpaka
unajifunza kupitia hayo na mwisho unapata yale uyatakayo duniani. Tukumbuke
maisha ni mara moja duniani, hatutaishi tena na jinsi tulivyo sasa”.
Kubali
vikwazo, ruka vihunzi ili uweze kwenda hatua nyingine mbele yako.
Na
Lusako Mwakiluma
No comments:
Post a Comment