Huwezi hata
kidogo kutenganisha maisha ya mwanadamu na elimu ya saikolojia, elimu ambayo
katika ulimwengu wa sasa wengi wanaisikia
lakini wachache wanaotambua umuhimu wake, achilia mbali maana ya neno
lenyewe. Mimi nimeona nikupe maarifa
haya baada ya kuona mwenyewe inanisaidia na pia kupitia Asasi ya WEZESHA TRUST FUND imewasaidia wengi na
watu wamepona magonjwa, wameshinda majaribu na leo hii wanafurahia kuifahamu
naomba na wewe uwe mmoja wao ambaye ukisoma mada hii utajua jinsi ya kuenenda.
Injinia
wa kwanza aliyeipa nguvu elimu hiii
ni mwanasaikolojia wa Kijerumani, Wilhelm Wundt ambaye alifungua
maabara na kutibu watu kwa kisaikolojia,
zoezi ambalo lilileta matokeo ya kushangaza ulimwengu mzima. Huo ulikuwa ni mwaka 1879.
Saikolojia ni
‘mtoto’ wa neno la Kigiriki lijulikanalo kama ‘psyche’ au akili na roho jina
ambalo baadae lilikuzwa na kufahamika
kama ‘Psychology’, tafsiri ikiwa
Elimu ya Nafsi na Ufahamu. Katika nchi zilizoendelea somo hili linapewa
nafasi ya juu katika maisha ya binadamu
kutokana na umuhimu wake. Wanasema wataalamu kuwa, kuishi bila kujua tabia za vitu na watu pia na ukuaji wake na kujifunza mabadiliko yake ni
sawa na kutembea katika kamba ndogo ya maisha salama. Unatakiwa ufahamu watu, wanyama, ndege na
vitu vinavyokuzunguka ili uweze kushinda majaribu au changamoto
zinazokuzunguka.
Saikolojia ni
somo ambalo kila kukicha binadamu anatakiwa kufundishwa kwa vile hakuna
anachoweza kukifanya kisiguse akili
na nafsi
yake. Inashauriwa kwamba ni lazima mtu ajifahamu mwenyewe pia awafahamu wengine, mazingira
anayoishi na mabadiliko yake wakati wote, tunaishi katika nyakati na majira na
unatakiwa ufahamu kila jambo linakupata linaanzia ndani yako mwenyewe. Unaweza ukalitengeneza bila kufahamu au
mazingira yakalitengeneza ukijua kabla haikusumbui.
Maswali ya
msingi yenye kumuongoza binadamu vizuri katika
maisha yake ni haya. Mimi ni nani, kwa nini niko hivi? Wale ni
watu ni akina nani? Kwanini
wako vile na tunapaswa kuwa vipi baadaye, pamoja na kujiuliza kwa
nini vitu vipo kama vilivyo.
Imebainika kwamba,
mvutano wa nguvu za dunia na za binadamu
huongezeka mara dufu kwa mtu ambaye hajui Saikolojia ya Maisha. Dunia kama sayari na mwanadamu kama kiumbe
kila mmoja amekuwa akitengeneza nguvu zake za kumuwezesha kuwepo, huku uzalishaji wa nguvu hizo kwa upande mmoja ukikinzana
vikali na mwingine, hata hivyo madhara makubwa
yamekuwa yakiwakuta binadamu
ambao ndani yao kuna uhai ambao ni sisi wenyewe.
Hata hivyo,
uchunguzi unaonyesha kwamba ufahamu,
nafsi na akili umebaki kuwa kinga muhimu ya mwanadamu katika ulimwengu huu ambao umekuwa unabadilika mara kwa mara. Hatari iliyokuwepo siku hizi ni hasa kwa ulimwengu huu wa tatu ni ukosefu wa
elimu hii muhimu, jambao ambalo limewafanya watu wenyewe kwa wenyewe kuzalishiana nguvu za
kuangamizana na kuiacha dunia ikishinda mara zote na watu kupoteza maisha
pasipo muda wao kufika au kuharibikiwa na mambo yao wakidhani ni hali ya kawaida.
Inahuzunisha pia kufahamu
kwamba mbali na binadamu
kushindana na mabadiliko ya ulimwengu na nguvu zake, wengi wao wamekuwa
wakipambana na nguvu zao wenyewe
ndani ya miili yao bila kujijua, kiasi
cha kupoteza maisha.
Tafiti za
wanasaikolojia zinaonesha kwamba asilimia kubwa ya matatizo
yanayomwangalia binadamu yanatokana na yeye mwenyewe au jamaa zake, huku ushahidi ukionesha
kuwa hata magonjwa ya kutisha kama moyo, kansa kisukari, vidonda vya
tumbo na mengineyo yanachangiwa na kiasi
kikubwa na mawazo ya mtu mwenyewe.
Magonjwa mengi hayapo ila watu wanayazalisha katika nafsi zao mwishowe
yanaenda kutokea kwa hofu zao na woga waliokuwa nao.
Karibu katika
Blog yetu uendelee kupata mambo mengine mengi muhimu ili uweze kujikwamua na
hali ya kushindwa na kuweza kushinda katika kila eneo la maisha yako na kupona
magonjwa yako yanayokusumbua kwa muda mrefu.
Na: Lusako
Mwakiluma Maheri
No comments:
Post a Comment