Tanzania
ni moja ya nchi ambayo imebahatika kuwa na rasilimali nyingi sana za aina
tofauti tofauti katika kila nyanja lakini sisi watanzania tumekuwa tukiendelea
kubaki katika hali ya kutojitambua na pindi wageni wanapokuja ndani
ya nchi wanatumia rasilimali tulizo nazo na wanapata upenyo wa kufanikiwa huku
tukiendela kuwaona kama wachawi. Kumbuka unapokiona wewe kitu hakifai na
kukidharau au kutokuwa na mtazamo sahihi ndipo inakuwa kuvuja kwa pakacha nafuu ya mchukuzi.
Katika
eneo hili tumejaribu kuangalia mambo machache ambayo yanaweza kukusaidia
kuweza kujitambua kuweza kusonga mbele katika maisha yao bila woga na
kujidharau huku ukijua faida yake katika siku zijazo. Ukiwa kama
ndugu, jamaa, rafiki unaweza ukaamua kufanya mabadiliko yako mwenyewe bila
kushurutishwa wala kulazimishwa na mtu.
1.Social
Yardstick(VIpimo vya Kijamii)
Muda
mwingine kwenye maisha yetu tumeshindwa kuzitumia fursa ambazo tunazo sababu
tumetumia jamii kama sehemu ya kipimo chetu cha kuendesha mambo na vitu vyetu. Mfano
Utasikia "Yaani mtoto wa fulani hakufanikiwa na alikuwa na akili sana wewe ndio
utafanikiwa?.Unaposikia hivyo mara nyingi watoto wetu wamedumaa na hata
akili zetu zimedumaa tumeshindwa kujua watu wengine ni wengine na sisi ni
sisi. Jaribu wewe mwenyewe usitumie mtu mwingine kama kipimo chako cha maendeleo."USIISHI KWA KUIGA HAUTAFIKA MBALI”
Kuitumia
jamii kama kipimo chako cha kuendesha vitu ni makosa jaribu kutumia uwezo wako
na nguvu zako ili kuweza kupiga hatua kwenye nyanja nyingi za maisha yako
binafsi hata ya familia yako. Mfano…"Mara nyingi familia nyingi zimetumia
watoto wengine kama kipimo cha malezi kwa watoto wa familia zao na sio wao kama
wao wanaweza kulea na kuwakuza watoto wao, uzuri au ubaya wa mtoto hautokani
kuwa mtoto wa jirani yako ni mzuri au mbaya".
2.Comparison(Kujilinganisha)
Hili
limekuwa miongoni mwa matatizo makubwa kwa tumetumia watu wengine kama sehemu
ya kipimo cha mafanikio ya fulani ingawa si vibaya kujua mwingine anafanya nini. Unapotumia
muda mwingi kujilinganisha na mwingine unapoteza uwezo wako halisi wa kufanya
vitu katika uwanda mpana wa maisha yako. Kumbuka kila mtu ana maono na ndoto
zake kwenye maisha yake unapojaribu kuwa kama yeye unaishi maisha yake wakati
wewe sio yeye. Jifunze kuishi maisha bila kujilinganisha linganisha na wengine
maisha ni kujaribu kutumia fursa zilizopo.Kumbuka unaweza ukafanya zaidi kuliko
mtu unayejilinganisha naye kwa kufanya zaidi na vizuri sana, hii inakuletea
hali ya kujiamini wakati wote. Na
kujifahamu kuwa wewe ni halisi.
Unaweza
ukajikuta unafanya vitu chini ya kiwango kumbe uwezo unao na huo uwezo unaweza ukawa ni mkubwa
zaidi ya hapo. Usiogope kuthubutu na
kujaribu na usiangalie nani anasema nini walioshindwa ndio waliofanikiwa. Jifunze katika kushindwa. Na walioshindwa wana maneno mengi ebu badilika na tumia kushindwa kwako kuwa ushindi kamili.
“Fikiria
Barak Obama, Hillary Clinton, Bill Gates, Les Brown, Napolean Hill, Ben Carson na wengine
wengi waliofanikiwa wangejilinganisha wangefika pale walipo.
Simama kwa nafasi yako na fanya kwa uwezo na nguvu zako zote bila hofu. Kumbuka riziki ya mbwa iko miguuni, akilala hawezi kupata anachotaka na wewe
jiangalie umetoka wapi na unaenda wapi endelea mbele ukiifuata hatima yako kwani wakati ni mali na kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe.
"ANGALIA FURSA KWA NAMNA YA KIPEKEE”
Na: Lusako Mwakiluma
No comments:
Post a Comment