Ukitaka kufanya kitu kisichowezekana lazima uwe na ndoto ya kutowezekana ndipo utakapoona hili ni tatizo na lazima litatuliwe. Tunapoenda kuangalia rekodi ya matukio au shughuli za mwaka kwa mwaka au katika rekodi ya historia kila mafanikio yametokana na hali ya kutowezekana kwanza na kulikuwa na hali ya changamoto ya ugumu wa mafanikio kabla na wengi walisema haiwezekani. Hapo ndipo ushindi unapatikana katika hali ya kutowezekana. Ebu mwangalie Alexander Braham Bell mfumbuzi wa kwanza wa kutengeneza simu au mawasiliano au Martin Luther King Jr au Susan B. Anthony ambaye alihakikisha wanawake wanapewa kibali cha kupiga kura au Nelson Mandela wa Afrika Kusini aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini baada ya kutoka jela na hakuna aliyejua kama atatoka kwa muda wote aliofungwa ni miaka mingi lakini iliwezekana na mtazamo wake au ndoto yake ilikuja kuwa ya kweli.
Wote hao waliendelea mbele huku wakijua haiwezekani huku
wakiwa na shauku ndani ya mioyo yao.
Ukitaka kupata kitu muhimu lazima uwe na kushindwa kwanza. Kitu usichowahi kukifanya hata siku moja
lazima uchechemee kwanza kabla haujafikia malengo. Hata mtoto anapozaliwa
lazima apitie kukaa, kutambaa, kusimama kisha kutembea hawezi kuzaliwa leo na
kuanza kutembea ikitokea hivyo basi itakuwa ni historia lazima iandikwe
magazeti na kwenye radio itangazwe. “Ukitaka
kupata kile ambacho haujawahi kukipata ni lazima ufanye kile kitu ambacho
haujawahi kukifanya” alisema Rais Obama wakati hajawa Rais akiwa kwenye maisha
ya kawaida sana na binti yake mmoja akiwa amemkumbatia pembeni ya gari bovu
mitaa ya uswahilini kabisa. Lakini leo
hii unamuona akiwa Rais na maisha bora yenye kutamanisha. Hajakurupuka Rais Obamaule alijipanga mpaka
kufika alipofika na leo hii anaheshimika ametimiza ndoto yake. Kumbuka mwenye
maono hafi mpaka ameyatimiza. Ukimuona
mtu mwenye maono amekufa bila kutimiza basi ujue hakuwa dhahiri katika ndoto
zake alikuwa mzungumzaji na sio mtendaji wa anachokisema na akishindwa yeye
basi hata mtoto wake anaweza kutimiza kama waliwahi kuongea na mwenye maono.
No comments:
Post a Comment