Kuna mtu anapitia maisha
ambayo yeye mwenyewe ukimuuliza hana majibu ya kukujibu, kwanza hajui kusudi la
maisha yake kwanini yupo na kwani nini anafanya kazi au kwanini anafanya
biashara. Utamkuta mtu anapata mshahara
milioni nne na mtu mwingine anapata mshahara laki tano, huyo wa laki tano
anaishi kwake hata kama ni chumba kimoja.
Sasa kama inafika mahali kila mtu analalamikia ugumu wa maisha na ikiwa
maisha sio magumu ila watu ndio wagumu. “Hauwezi
kuibadilisha dunia ila inabidi ubadilike wewe binafsi ndio utaona mabadiliko
kwenye jamii inayokuzunguka”
Hivyo basi ndugu zangu ebu
tuanze kubadilika mbona tunaweza kuchangia sana harusi na shughuli ambazo sio
rasmi lakini kwenye maswala ya maendeleo yetu binafsi tunakuwa wagumu. Mshahara ni pesa na zinazoesabika mtu
anapopata pesa nyingi nae anaongeza matumizi mengine zaidi.
Naomba tubadilike ili
tujipange na kuhakikisha changamoto za maisha tunazikabili badala ya kupiga
kelele na kuimba kila siku hali ni ngumu.
Chochote unachokiwaza ndicho kitakuja kama unawaza kushindwa basi
kushindwa ndio fungu lako, kama unawaza kufanikiwa basi mafanikio yatakuwa ya kwako kwa kiasi
unachotaka.
Naamini tutabadilika na
kuweza kuwa wabunifu wazuri wa kufanya vitu na watu wa kuwaiga ni wale
waliofanikiwa hata tuweze kuwahoji wamefikaje hapo walipofika ili nasi tuanze
michakato ya kujikwamua na hali tunazozipitia kwani hata mbuyu ulianza kama
mchicha. Badala ya kujiinamia ni kukaa
chini na kutafakari nini kifanyike ili tuweze kupanga mwanzo ili tufikie mwisho
mzuri wenye mafanikio na matunda.
Naamini kwa yeyote mwenye
nia njema ya kubadilisha maisha yake basi tuwasiliane ili tuweze kupeana
ushuhuda wa mafanikio na kuelekezana tunatakiwa kufanya nini ili kuweza
kuyapata yale ambayo tunayaona ni magumu kuyapata. Kwani hata Obama alisema “ukitaka kupata ambacho haujawahi kukipata
utakiwa kufanya yale ambayo haujawahi kuyafanya”.
Nakutakia usomaji mzuri wa makala
zangu.
Lusako Mwakiluma
No comments:
Post a Comment