Elimu ni ufunguo wa maisha, na
elimu siku zote huwa haimtupi mtu: Kwenye Mithali 4:13 unaambiwa mkamate
sana elimu, usimwache aende zake; mshike, maana yeye ni uzima
wako.
Nahamasika kuwakumbusha
watanzania wenzangu, maarifa ni jambo jema sana na watanzania inabidi tujifunze
sana kupitia vijarida, majarida, vitabu na vitu vinatuhamasisha kujua ukweli na
mambo ya dunia inavyokwenda katika ulimwengu wa leo. Dunia inabadilika haraka sana na mimi binafsi
naliona hilo naamini hata watanzania wenzangu wanaliona hilo.
Ebu tuwekeze kwenye kujisomea vitabu
mbalimbali au vijarida kama wewe ni mvivu basi soma kwa siku kurasa kadhaa
zenye kukupa kitu kipya na watu wenye mambo mazuri huwa wanayaweka kwenye
maandishi. Na sio kufanya mawasiliano ya
kuandikiana jumbe fupi fupi zenye kuulizana huko wapi unafanya nini, au basi
turushiane mambo yenye kututoa sehemu moja kwenye nyingine. Ebu turudi pale pale kwenye maneno ya Mungu
kwani unaambiwa katika Mithali 3:20 Enenda na wenye hekima na wewe utakuwa na
hekima lakini rafiki ya wapumbavu hataangamia.
Basi ebu tuchague marafiki wa kutembea nao au kufanya nao kazi,
utamchaguaje mtu ambaye afikirii maendeleo yeye muda wote anataka mkae chini muanze
kujadili mambo ya watu??
Ndugu, siwezi kutumia lugha ya
kukulazimisha ila tushirikiane kwa pamoja kuhakikisha tunasimama katika nafasi
zetu ili kuhakikisha kwamba tulipo tunahama na kuhamia mahali pa juu
palipoinuka. Kuna mtu ananiambia mimi
siwezi kujiendeleza nikamuuliza kwanini, akasema nilipo hapa ofisini hata
nikijiendeleza siwezi kupandishwa cheo, siwezi kupewa nafasi sahihi kwa
nilichosomea nikamwambia unaujua wakati wa MUNGU?
Basi napenda nikushirikishe
elimu ni yako binafsi na mafunzo ndiyo ya kupewa na taasisi au na msaidizi wako
au nduguzo. Kwanini nimesema hayo? Elimu inaanzia ya awali mpaka ya Chuo Kikuu na
hii elimu ni kwa manufaa yako binafsi na si mtu mwingine na sio lazima elimu
yako ikusaidie wewe inaweza kuwasadia watu wengine wala sio wa kwenye taasisi
yako au shirika lako. Haya basi
umestaafu na wewe ni Prof. wa Chuo ulani
huo Uprofessor hauwezi kuwafundishwa wengine wa chuo kingine au jamii
inayokuzunguka? Jana wakati unasoma
uliona ni ya kwako binafsi lakini leo hii unaona inavyokusaidia.
Basi tuanze sasa na
tusiangalie tuna umri gani, elimu haina mwisho, na elimu ni hazina na elimu ni
ufunguo wa maisha yetu ya kila siku.
Karibuni
Lusako
Mwakiluma
No comments:
Post a Comment