Watu
wangapi wana malengo mazuri katika maisha yao?
Watu wote tunayo. Sasa ni
wangapi wanaongelea hata lengo moja
zuri? Hawawezi hata kuongelea lengo
ambalo litaweza kumbadilishia maisha yake.
Watu wengi wanakata tamaa hata hawataki hata kujaribu, wanaanza kulalamika
tu mimi siwezi, mimi sitaweza hali hii
ilimkuta Sir Edmund Hillary aliulizwa
kwenye mahojiano alipata changamoto gani alipokuwa mtu wa kwanza kufika kwenye
kilele cha Mlima Everest? Akasema
changamoto kubwa aliyoipata ni ya
kisaikolojia ambayo ilikuwa inamsumbua
kutoka kuongea mpaka kuthubutu kwa
kusema “Sitaweza” na “Haitawezekana”.
Hivyo
basi changamoto kama hii inawapata wengi kwa kukata tamaa kabla hawajajaribu
kufanya kitu. Muda wote tunaona hatuwezi
kwa sababu hatutaki kujaribu. Sir Edmund Hillary alifika juu ya kilele cha mlima
Everest na akaonyesha inawezekana na baadae ikawa rahisi kwa wengine. Mwingine nae baada ya kuona imewezekana kwa
Sir Hillary nae anasema ngoja nami niupande mlima huu. Sasa hivi hata watalii wengi tu wanaupanda mlima Everest bila hofu yoyote sio mlima
mpendwa msomaji ila ni sisi wenyewe ndio
mlima.
Kila
wakati unamaliza jambo hata likiwa dogo, unaongeza na hali yako mwenyewe ya
kufanya, pia unapiga picha yako, pia
unaongeza na mawazo yako. Unaweka akiba kidogo
ya ujasiri. Unasema kutokea
ndani, “Niko sawa” “niko sawa” angalia navyofanya!!! Kila utakavyofanya hivyo basi unaweza kufanya kitu zaidi na zaidi. Inaanza kidogo kidogo mpaka unamaliza kufanya jambo kubwa
sana!!! Lakini kumbuka inaanzia kwako,
amini mwenyewe na ondoa adui wa ndani
yako ambaye anasema siwezi na yeye akikubali basi kila kitu kinakuwa sawa!!!
Adui
wa pili anayeua ndoto yako ni kusumbukia vitu vidogovidogo, au kukaa na watu
wanaosema haiwezekani. Wote wanaotumia
neno haiwezekani au siwezi unawajua, hauwezi kufanya haya wewe ni mzee, hauwezi
kufanya hivi kwa kuwa hauna elimu ya kutosha, hauwezi kufanya lazima uwe na sifa hizo kwanza hapa hauna
sifa kulingana na kazi yenyewe, hauwezi kufanya kazi hivyo inaonyesha jinsi
gani ukate tamaa na kuacha kufikiria makubwa.
Hauwezi! Hauwezi! Hauwezi!! Acha hiyo hali ya
huzuni, unaweza kufanya kitu
chochote ni kweli kama unataka
kufanya. Kama una ndoto na ukaifuata
ndoto yako. Basi hakikisha unaifikia hiyo ndoto kama
ulivyoota. Usiangalie watu wanasema nini na wanakuonaje kwa nje kama ipo ipo tu
lazima itimie!!!!!!!
Na Lusako Mwakiluma
No comments:
Post a Comment