Watu
wengi wanaongea kuhusu kusubiria meli yao ije ili waingie ndani. Wametulia na
kusubiria muda ufike. Nakumbuka katika
siku zangu wakati naimba pale kwenye ukumbi fulani nilikuwa nasubiria muda
ufike ili nipumzike. Baadae nikasikia
watu wanazungumza na kusema endelea kuimba, endelea kuimba,
endelea kuimba kuna muda utafika na utapumzika tu. Niliendelea kusubiria mapumziko yangu lakini
hayakutokea. Baadae nikaanza kujifunza kwamba mafanikio ni uamuzi wa mtu na sio kitu kinachotokea kwa
bahati kwa binadamu yeyote.
Nimejifunza
kwamba njia nzuri ya kukua katika maisha
ni kuanza kukua kwako binafsi. Ninaanza
na kipindi cha mandeleo yangu binafsi na
nimeamua kwamba sitaweza kusubiria
mapumziko yaje. Nitakwenda kujiwekea mapumziko yangu mimi mwenyewe. Nina uamuzi wangu. Sitaendelea
kusubiria meli yangu ije niingie au itabidi
niogelea na kuifuata uko iliko. Ninafuraha kwamba nimefanya kwasababu marafiki zangu
wengi wameendelea kusimama na kuendelea kusubiria meli yao ifike ili waingie.
Jonathan
Winters alisema, “Nilisubiria mafanikio lakini sikuyaona, nikaamua kwenda bila
mafanikio” Folks alisema, “Mafanikio sio
kitu cha kusubiria…. ni kitu ambacho unatakiwa lazima ukikamilishe na
ukipate!!! Usisubirie meli yako ije na uingie…. ebu ingia ogelea na uikute hiyo
meli ili upande na uendelee na safari yako!!!! Utafurahia sana kufanya hivyo
mara utakapojitambua. Ebu amka na uanze
kuogelea uikute meli yako rafiki, ndugu, mpendwa wangu muda haukusubiri
wewe. Ingia ndani ya maji uanze kuogelea
uifuate meli yako popote ilipo na uende safari yako.
Na: Lusako Mwakiluma
No comments:
Post a Comment