Friday, March 28, 2014

IMANI NA UJASIRI VS HOFU NA WASIWASI



Michael Kelly ni msemaji na pia ni mkufunzi kutokea  Virgina Beach Va,  watu wanapenda kumwita “Professor” kwa sababu  ya mawazo na  habari anazopenda kuongea na watu akiwaamasisha.  Katika shughuli zake, Michael  alisema habari ya  nguvu kuhusiana na tofauti kati ya  imani na ujasiri pamoja nahofu na wasiwasi napenda na wewe nikujulishe zaidi ili tubadilishane mawazo.

Kuna wakati kulikuwa na vijana wawili. Hofu na wasiwasi walikuwa wanakwenda katika kila nyumba na kugonga mlango. Wakati watu walipokuwa wanafungua mlango waliingia ndani na kuhakikisha wanatikisa kisawasawa juu kwenda chini. Kuleta migongano, ndoa kuharibika na amani kutoweka. Hofu na wasiwasi anaendelea kwenda nyumba hadi nyumba, kutoka mji hadi mji mwingine na kutoka nchi hadi nchi nyingine kuharibu matumaini ya watu na ndoto zao.  

Siku moja hofu na wasiwasi walikuja katika sehemu mpya na wakakuta nyumba kubwa sana na kusema; “ Ebu twende pale twende tukafanye uharibifu”  Hofu na wasiwasi wakafika mlangoni na kuanza kugonga, lakini hawakujua  kwamba hii ni nyumba ya adui yao hofu na wasiwasi, hofu na wasiwasi  wakagonga kwa nguvu na bidii mwisho wakawa na hasira.  Mwishoni kabisa imani na ujasiri wakafungua mlango na walipofungua mlango…. hawakuona mtu yeyote aliyegonga pale!!! Wakatoka nje wakaangalia  mpaka mtaa wa pili hakuna mtu, na wakaanza kuangalia mtaa mwingine tena hakuna mtu anayegonga kwa sababu katika uso wa imani na ujasiri…. hofu na wasiwasi siku zote  zinaondoka zenyewe na mtu aliye na hofu na wasiwasi hawezi kumtikisha mtu jasiri na mwenye imani ya kweli.

Hali ya mwisho ya muua ndoto ni  kufanya vitu vya hali ya kiwango cha  chini, na kama kutakuwa na hali nzuri basi  itabidi hatua ipigwe na kwenda mbele tu wakati wote.  Huyu muua ndoto yuko sana kwa vijana wetu ambao wanadanganywa na kuamini  kuwa maisha yanatokana na haraka na kupata vitu haraka kabla ya muda haujafika na katika vijana wanafikiria sana leo badala ya kesho yao!!! 

Katika watu wazima  hali ya kiwango cha chini katika  katika kazi zao  ni sawa na kusema, “Hii inatosha”.  Wanajiwekea mipaka kwamba hii inatosha wakati hali ya ubora au uzuri wa jambo  lazima ukamilike kwa kuongeza nguvu wakati wote.  Watu wengi wanapenda vitu vidogo vidogo wala hawana ndoto kubwa ukiwauliza wanakwambia je, nikifa kesho watu wagombee mali zangu au kwanini nijichoshe na kuandika kitabu kitanisaidia nini, na kwa nini  muda wote tu najisomea tu natakiwa nipumzike,  lakini kumbuka  watu hawawezi kusahau ulivyowafanyia wakawa na amani siku zote aidha kwa kupitia maneno ya kinywa chako au kupitia majarida au vitabu vyako siku zote!!!  Amka ndugu yangu muage hofu na wasiwasi mtafute imani na ujasiri akae na wewe siku zote za maisha yako!!!!!

Na: Lusako Mwakiluma

No comments:

Post a Comment