Leo
nataka nikwambie kitu ambacho nimekisoma
katika kitabu cha mafanikio hayawezi
kwisha na kushindwa hakuna mwisho
alisema Dr. Robert Schuller. “Usiogope
hata kama utakosea amini katika
ndoto yako. Usihofu kama
hautakwenda kwa ajili ya ndoto yako utakuwa
umesimama kabla Mungu hajakwambia nenda kaendelee na kama imani yako ni ndoto basi utapata
imani zaidi.
Hofu ya
kufikiria kushindwa. Hofu inayokwambia
hauwezi kufanikiwa, na kama hautajaribu basi hautaweza kupata changamoto. Hofu wakati mwingine inaumiza. Hofu itakusababisha usikue na kama utasubiri kupata maumivu ya mafanikio.
Rafiki
usihofu ila nenda na ndoto yako. Kuna mtu mmoja zamani alisema na kijana mdogo
kama utakutana na hofu. Usiogope ni ngumu kufikia namba mbili kama
hata namba moja haujaikamilisha. Una
ndoto yako jaribu kuitendea kazi hiyo ndoto kisha utapata mambo makubwa sana.
Usiogope hofu si kitu kabisa. Ni hali
inayopita tu kwani hofu ikiingia ndani yako basi jua kuna hali ya magonjwa
itainuka ndani yako kama kisukari, BP na vidonda vya tumbo, maumivu ya kichwa
na magonjwa mengi.
Wote tuna
hofu, na tumezaliwa hivyo na sisi wenyewe ndio
tunaoweza kuhakikisha hali hii inaondoka kwa kufanya maamuzi na kuogopa
hatari, ila hofu haimaanishi kwamba inaweza kutuwekea vipingamizi ili
tusifanikiwe na kufanya mambo
makubwa. Tuna maamuzi kama tuna imani na kuamini au imani yetu au
uwezekano wetu. Kama rafiki, ndugu,
mpendwa tushirikiane kuona hofu inavyofanya kazi na asiye na hofu
anavyofirikia.
Hofu inaona
changamoto. Imani inaona fursa
Hofu inaona
matatizo. Imani inaona jinsi ya kufikia ndoto
Hofu inaona
kuna ukuta mzito. Imani inaona kuna njia
ya kutokea
Ni uamuzi
wako, unaweza ukawa na imani katika hofu au
katika upande wetu. Ebu kuwa na
imani!! David Schwarz aliandika: hali ya kufikia makubwa ni hali ya kuponya hofu kwa vitendo. Ebu
elezea hofu na kisha endelea mbele.
Chukua hatua na kisha hofu yenyewe itaondoka.
Je, una imani, ebu fanya kwa vitendo na hiyo “HOFU ITAONDOKA”.
No comments:
Post a Comment