Wednesday, April 2, 2014

MSAADA JAMANI KUMSAIDIA MWENZETU ILI APATE MATIBABU HARAKA             Mpendwa Mtanzania mwenzangu, rafiki, mdogowangu na yeyote atakayeguswa

YAH:  MAOMBI YA FEDHA KUMSAIDIA ASHA MANGA MATIBABU MUHIMBILI
            TSHS. 4,000,000/=

Tafadhali rejea kichwa cha habari hapo juu.

Asha Manga ni msichana mwenye umri wa miaka 25 ametokea Mkindo Turiani anasumbuliwa na maumivu ya Taya tangu mwaka 2008, alipata uvimbe mdogo mwaka huo uliompelekea kuanza kuota nyama ndani ya kinywa chake na kumletea  maumivu makali wakati wote hawezi kuongea na anakula vitu laini tu na vya majimaji.

Asha ni mkulima na anaishi na mama yake huko Turiani ambaye ni mzee na anamtegemea Asha ambaye ndiye alime ili alete mahitaji.  Mwaka huu kwa maumivu Asha ameshindwa kufanya chochote kwani hali inazidi kuwa mbaya na uvimbe unazidi kuongezeka. Kwa sasa Asha ninaishi nae nyumbani kwangu kwani hapa Morogoro mjini Asha hana ndugu yeyote  wa kuweza kumsaidia.

Ewe mtanzania mwenzangu, mwanajamii watanzania wenzangu, marafiki, ndugu, jamaa na yeyote utakayeguswa na tatizo la huyu msichana naomba tumsaidie ili  akafanyiwe upasuaji wa kubadilishiwa taya pale Muhimbili kwani hali ya Asha inakatisha tamaa sana na Daktari amemjulisha hali hii ikiendelea itabadilika na kuwa kansa kitu ambacho hakitakubali upasuaji tena. Kiasi cha pesa kinachotakiwa ni Tshs. 4,000,000/=.   Soma Zaburi 41:1   Heri amkumbukaye mnyonge; Bwana atamwokoa siku ya taabu. 

Natanguliza shukrani za dhati na Mungu atakubariki sana kwa kusimama na kulia na wanyonge.  Kwani Asha bado ni msichana mdogo sana na tunamhitaji sana kuongeza nguvukazi ya Taifa letu.   
Nimeambatanisha picha ya Asha kuonyesha uvimbe uliopo mdomoni mwake.  Mungu atakubariki kwa kutoa kwa kadri ulivyojaaliwa, unaweza kutumia akaunti namba ya Wezesha Trust Fund (CRDB)-0152392951200 au MPESA 0767448186  & TIGOPESA 0713448181.


                                                    Nawasilisha kwenu wanajamii wenzangu.

Lusako Mwakiluma Maheri
Mkurugenzi
WEZESHA TRUST FUND

1 comment:

  1. pamoja na michango tumuombee mungu amjaalie kupona haraka jambo ambalo mimi naamini linawezekana

    ReplyDelete