Friday, April 11, 2014

UNAWEZA KUMPELEKA PUNDA KUNYWA MAJI NA WALA ASINYWE MAJI





Unaweza kumpeleka punda kunywa maji na wala asinywe hayo maji, unaweza kumtwanga mpumbavu kwenye kinu na wala upumbavu wake usimwishe.   Kuna habari ya  ya mtu mmoja yeye alikuwa anataka  kujua siri ya mafanikio.  Alikwenda kumuona mtu mwenye busara, “Akamuuliza nifanyeje ili niwe na mafanikio?”.   Mzee mwenye busara akajibu akasema; “ Unatakiwa ubadilishe kufikiria kwako  kisha ubadilishe matendo yako na mwisho  uwe tayari  kufanya vitu fulani vitakavyokufanikisha”  Yule mtu akatulia  na kufikiria maneno ya mwenye busara na tena akaondoka.   Hakutaka kubadilisha kufikiria kwake, akutaka kufanya hayo yote kwani aliona kuna mambo yake yataharibika kwa kubadilisha yaliyo kwenye fikra zake, alikuwa mbishi kubadilika na kwahiyo aliamua kushindwa.  Ndugu zangu waume kwa wanawake, ilikuwa ni wakati ule wa zamani.   Je! wewe unafikiria nini, Ebu badilisha kufikiria kwako na pia badilisha maisha yako kwa kuwa tayari kuthubutu na kufanya kitu unachotaka kufanya kwa wakati!!!!

Tunafika mahali tunafikiria.  Kile unachokifikiria  ndiyo kitakusababisha ufanye na malengo yako yatakwenda badala yake.  Wote wanaofikiria kuhusu malengo yao  ni wale wanaofikia malengo, ila wale  wote wasiofikiria kitu nao hawawezi kufanya kitu.  Wote wasiokuwa na wazo   wanaenda kuwa na fikra zilizochangamana na hofu, wasiwasi na woga.  Tangu walivyofikiria hivyo wanaenda kupata hayo; wamejazwa na michanganyo vichwani mwao, hofu, wasiwasi na woga.  Kama  unafikiria hauna kitu,  lazima hutakuwa hauna kitu; ukifikiria makubwa, lazima upate makubwa.

Na Lusako Mwakiluma

No comments:

Post a Comment