Wednesday, April 23, 2014

NGUVU YA MAAMUZIMuda gani inakuchukua kubadilisha maisha yako.  Watu wengi wanaamini kwamba ni muda mrefu sana sio kweli ni siku moja tu ya kufanya maamuzi.  Ni kweli masaa 24 tu yanaweza kubadilisha maisha yako  kabisa kabisa.  Kwanini inakuchukua muda mrefu kufanya maamuzi?  Imefika mahali unaamua halafu  unakata tamaa.  Unajua ndege inapoanza kupaa huwa inachukua kasi na ikishachukua kasi inaanza kutafuta usawa wa kuruka kwenda juu.  Rafiki yangu ikishashika kasi hata kama umesahau kitu rubani hawezi kusimama au kurudi na kuchukua ulichokiacha ni safari mpaka ifike mwisho wa safari yake. 

Ndivyo na wewe unavyotakiwa kuwa kwamba, ukiamua sasa naanza safari ya mabadiliko ya maisha yako hakuna kugeuka nyuma kumbuka Ruthu aligeuka nyuma akawa jiwe la chumvi ina maana kama uliwahi kufanya biashara huko nyuma ukafilisika usigeuke kukumbuka magumu ya ile biashara hii ni biashara mpya soma Isaya 43:18 katika maandiko ya biblia takatifu -Nanukuu:Msiyakumbuke  mambo ya kwanza wala msiyatafakari mambo ya zamani. “In English don’t talk about the past, live today live fully”.  Mtu anaweza kuwa na wazo la mabadiliko akakaa nalo muda mrefu sana baadae lile wazo lake likafa kabisa na kupotea kwa sababu hakuchukua maamuzi.  “Ideas goes away direction stays”.  Kama muda wa mabadiliko umefika lazima uchukue maamuzi thabiti na kuanza kwenda mbele bila hofu yoyote.

Dr Howard Thurman Theologia mkubwa ulimwenguni alisema kwenye hotuba zake “kwa wakati kila dakika unayozalisha hofu ndio muda  unaoruhusu adui kushinda”.   Majaribu yanakuja  lakini unamruhusu adui kushinda” Muda unapoamua  kuchukua maamuzi  sahihi na kwenda mbele na maamuzi yako ni kwenda kubadilisha maisha yako”  Adui hana nafasi akikuona una hofu wala kuyumba anabaki anajiuliza kuna nguvu gani ndani yako?  kumbuka pia wewe ni mfano wa Mungu iwe una imani tofauti bado  Mungu ni wa wote na ana ukuu katika maisha yetu.  Kuna marafiki zangu Fortune na Glory wao walikuwa na semina, walivyoanza semina yao walianza na swali “unakwendaje kufanikiwa katika maisha yako” wahudhuriaji walibaki wakiguna na kuulizana bila majibu yoyote: Jim na Naomi  walijibu swali na kusema ni “kuamua tu” Umuhimu wa kubadilisha maisha yako ni suala la kuamua tu.

Og Mandino aliiita “Siri ya kuamua” Les Brown aliita “ni hali ya kuamua” Anthony Robbins aliita “mwisho wako unategemea na maamuzi yako”. Hivyo unataka uwe hivyo? Umuhimu wewe ni nani na huko wapi? Na hapo ulipo upo kwa sababu ya kuamua kushinda au kushindwa kufanya maamuzi.  Amua maisha yako kabla maisha hayajaamua badala yako.  Tunatakiwa tuongoze maisha yetu kwa kufanya maamuzi ya kuchagua jinsi gani tuishi. Maamuzi yako ndio siku utakayobadilisha maisha yako “uamuzi ni ufunguo wa kubadilisha maisha yako” Hivyo fanya maamuzi leo kwanza ili ujue wapi unatakiwa kwenda? Kwanza lazima uwe na mtazamo au ndoto!!!

No comments:

Post a Comment