Thursday, July 3, 2014

ANGALIA FURSA KWA NAMNA YA KIPEKEE (SEEING WHAT OTHERS DON'T)

Leo nakuletea mada ambayo inaweza kutusaidia kubadilisha mfumo wetu wa kufikiri na namna ambavyo tunaweza kuangalia vitu kwa namna ya pekee.

Tanzania ni moja ya nchi ambayo imebahatika kuwa na rasilimali nyingi sana za aina tofauti tofauti katika kila nyanja lakini sisi watanzania tumekuwa tukiendelea kubaki katika hali ya kutojitambua na pindi wageni wanapokuja ndani ya nchi wanatumia rasilimali tulizo nazo na wanapata upenyo wa kufanikiwa huku tukiendela kuwaona kama wachawi. Kumbuka unapokiona wewe kitu hakifai na kukidharau au kutokuwa na mtazamo sahihi ndipo inakuwa kuvuja kwa pakacha nafuu ya mchukuzi.

Katika eneo hili tumejaribu kuangalia mambo machache ambayo yanaweza kukusaidia kuweza kujitambua kuweza kusonga mbele katika maisha yao bila woga na kujidharau huku ukijua faida yake katika siku zijazo. Ukiwa kama ndugu, jamaa, rafiki unaweza ukaamua kufanya mabadiliko yako mwenyewe bila kushurutishwa wala kulazimishwa na mtu.

1.Social Yardstick(VIpimo vya Kijamii)
Muda mwingine kwenye maisha yetu tumeshindwa kuzitumia fursa ambazo tunazo sababu tumetumia jamii kama sehemu ya kipimo chetu cha kuendesha mambo na vitu vyetu. Mfano Utasikia "Yaani mtoto wa fulani hakufanikiwa na alikuwa na akili sana wewe ndio utafanikiwa?.Unaposikia hivyo mara nyingi watoto wetu wamedumaa na hata akili zetu zimedumaa tumeshindwa kujua watu wengine ni wengine na sisi ni sisi. Jaribu wewe mwenyewe usitumie mtu mwingine kama kipimo chako cha maendeleo."USIISHI KWA KUIGA HAUTAFIKA MBALI”

Kuitumia jamii kama kipimo chako cha kuendesha vitu ni makosa jaribu kutumia uwezo wako na nguvu zako ili kuweza kupiga hatua kwenye nyanja nyingi za maisha yako binafsi hata ya familia yako. Mfano…"Mara nyingi familia nyingi zimetumia watoto wengine kama kipimo cha malezi kwa watoto wa familia zao na sio wao kama wao wanaweza kulea na kuwakuza watoto wao, uzuri au ubaya wa mtoto hautokani kuwa mtoto wa jirani yako ni mzuri au mbaya".

 2.Comparison(Kujilinganisha)
Hili limekuwa miongoni mwa matatizo makubwa kwa tumetumia watu wengine kama sehemu ya kipimo cha mafanikio ya fulani ingawa si vibaya kujua mwingine anafanya nini. Unapotumia muda mwingi kujilinganisha na mwingine unapoteza uwezo wako halisi wa kufanya vitu katika uwanda mpana wa maisha yako. Kumbuka kila mtu ana maono na ndoto zake kwenye maisha yake unapojaribu kuwa kama yeye unaishi maisha yake wakati wewe sio yeye. Jifunze kuishi maisha bila kujilinganisha linganisha na wengine maisha ni kujaribu kutumia fursa zilizopo.Kumbuka unaweza ukafanya zaidi kuliko mtu unayejilinganisha naye kwa kufanya zaidi na vizuri sana, hii inakuletea hali ya kujiamini wakati wote.  Na kujifahamu kuwa wewe ni halisi.

Unaweza ukajikuta unafanya vitu chini ya kiwango kumbe uwezo unao na huo uwezo unaweza ukawa ni mkubwa zaidi ya hapo.  Usiogope kuthubutu na kujaribu na usiangalie nani anasema nini walioshindwa ndio waliofanikiwa.  Jifunze katika kushindwa.  Na walioshindwa wana maneno mengi ebu badilika na tumia kushindwa kwako kuwa ushindi kamili.

“Fikiria Barak Obama, Hillary Clinton, Bill Gates, Les Brown, Napolean Hill, Ben Carson na    wengine wengi waliofanikiwa wangejilinganisha wangefika pale walipo. 

Simama kwa nafasi yako na fanya kwa uwezo na nguvu zako zote bila hofu.  Kumbuka riziki ya mbwa iko miguuni, akilala hawezi kupata anachotaka na wewe jiangalie umetoka wapi na unaenda wapi endelea mbele ukiifuata hatima yako  kwani wakati ni mali na kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe.

 "ANGALIA FURSA KWA NAMNA YA KIPEKEE

Na: Lusako Mwakiluma

No comments:

Post a Comment