Wednesday, August 20, 2014

MTAZAMO UNABADILISHA KILA KITU Mpendwa msomaji wa mada zangu napenda nikwambie kitu, mtazamo ni kila kitu, unaweza ukatazama ng’ombe ukamuona simba kwa jinsi unavyoona wewe ndivyo unavyotengeneza kuhamisha kitu katika fikra zako, anza leo hii kutazama kwa jicho la ndani.


Ebu ona ushindi na baki ukifikiria ushindi wa hali ya juu, simamia mtazamo na uone jinsi unavyoweza kubadilisha maisha yako kwa haraka zaidi.  Kwani fikra ndio kila kitu ulizoea kuwaza mabaya leo hii unaanza kufikiria mazuri  na utaona uzuri ukikusogelea.


Angalia waliofanikiwa, waulize walipitia wapi na nini mpaka wakafikia hapo,  tazama kwa jicho la tofauti yaani jicho la ndani yako tokea moyoni mwako huku ukiwa na shauku ya mabadiliko ya hali ya juu.


Ongea na moyo wako, ongea na kioo chako, ongea ndani ya gari yako, ongea katika chumba chako cha siri utaona jinsi mabadiliko yanavyoenda kutokea kwa kupata shauku nzuri ya kukubadilisha na kuwa mtu mpya na wa tofauti kwa kuwaza chanya kila siku katika jamii na maisha yako kwa ujumla.

Karibu tuendelee kutiana moyo, kuinuana kila wakati.

Na: Lusako Mwakiluma

No comments:

Post a Comment