Thursday, January 30, 2014

MAISHA NA CHANGAMOTO



Kuna mtu anapitia maisha ambayo yeye mwenyewe ukimuuliza hana majibu ya kukujibu, kwanza hajui kusudi la maisha yake kwanini yupo na kwani nini anafanya kazi au kwanini anafanya biashara.  Utamkuta mtu anapata mshahara milioni nne na mtu mwingine anapata mshahara laki tano, huyo wa laki tano anaishi kwake hata kama ni chumba kimoja.  Sasa kama inafika mahali kila mtu analalamikia ugumu wa maisha na ikiwa maisha sio magumu ila watu ndio wagumu.  “Hauwezi kuibadilisha dunia ila inabidi ubadilike wewe binafsi ndio utaona mabadiliko kwenye jamii inayokuzunguka”

Hivyo basi ndugu zangu ebu tuanze kubadilika mbona tunaweza kuchangia sana harusi na shughuli ambazo sio rasmi lakini kwenye maswala ya maendeleo yetu binafsi tunakuwa wagumu.  Mshahara ni pesa na zinazoesabika mtu anapopata pesa nyingi nae anaongeza matumizi mengine zaidi. 

Naomba tubadilike ili tujipange na kuhakikisha changamoto za maisha tunazikabili badala ya kupiga kelele na kuimba kila siku hali ni ngumu.  Chochote unachokiwaza ndicho kitakuja kama unawaza kushindwa basi kushindwa ndio fungu lako, kama unawaza kufanikiwa  basi mafanikio yatakuwa ya kwako kwa kiasi unachotaka.

Naamini tutabadilika na kuweza kuwa wabunifu wazuri wa kufanya vitu na watu wa kuwaiga ni wale waliofanikiwa hata tuweze kuwahoji wamefikaje hapo walipofika ili nasi tuanze michakato ya kujikwamua na hali tunazozipitia kwani hata mbuyu ulianza kama mchicha.  Badala ya kujiinamia ni kukaa chini na kutafakari nini kifanyike ili tuweze kupanga mwanzo ili tufikie mwisho mzuri wenye mafanikio na matunda.

Naamini kwa yeyote mwenye nia njema ya kubadilisha maisha yake basi tuwasiliane ili tuweze kupeana ushuhuda wa mafanikio na kuelekezana tunatakiwa kufanya nini ili kuweza kuyapata yale ambayo tunayaona ni magumu kuyapata.  Kwani hata Obama alisema “ukitaka kupata ambacho haujawahi kukipata utakiwa kufanya yale ambayo haujawahi kuyafanya”. 

Nakutakia usomaji mzuri  wa makala zangu.

Lusako Mwakiluma

No comments:

Post a Comment