Tuesday, March 18, 2014

CHAGUA KUWA NA FURAHANiliangalia katika television  ilikuwa inaonyesha mtu mmoja ambaye alikuwa anasema kuna  maamuzi mawili ambayo kila mtu asubuhi ukiamka unatakiwa kuyachagua ili uwe na amani!!!

Akasema: Unatakiwa kuchagua kuwa na furaha au kuwa na huzuni.  Mtu  huyo yeye alichagua kuwa na furaha kwa sababu furaha ni hali ambayo iko ndani ya mtu na inaanzia ndani. Kwa hiyo unapoamka asubuhi furaha izae ndani yako kila siku.  Kwani kila siku kuna fursa ambayo itabidi uipokee.   

Na kuna wengine wanaamka na hali ya chanya katka ufahamu wao na  pia wanakuwa na hali ya chanya kabisa  na kusema “Asubuhi njema asante Mungu wangu!!!!  

Wakati wengine wanaamka na hali ya huzuni  na pia kwenye ufahamu wao wameujaza huzuni wa hali ya juu. Na kusema Mungu hii asubuhi chochote unachotaka kuamua kuhusu mimi  na kiwe tu. 

 Naomba ndugu yangu uamue kuamka asubuhi na kumwambia Mungu asubuhi ni nzuri sana  kwa sababu kila kitu ni kizuri kwangu (alisema Ziglar) kama hauamini ebu jaribu uone.  Unapoamka lazima uhesabu baraka ili uweze kuwa na furaha. 

 Ndugu maamuzi ni yako!!!!

Na lusako Mwakiluma

No comments:

Post a Comment