Thursday, March 20, 2014

HAKUNA MLIMA, ILA MLIMA NI SISI WENYEWEWatu wangapi wana malengo mazuri katika maisha yao?  Watu wote tunayo.  Sasa ni wangapi  wanaongelea hata lengo moja zuri?  Hawawezi hata kuongelea lengo ambalo litaweza kumbadilishia maisha yake.  Watu wengi wanakata tamaa hata hawataki hata kujaribu, wanaanza kulalamika tu mimi siwezi, mimi sitaweza  hali hii ilimkuta Sir Edmund  Hillary aliulizwa kwenye mahojiano  alipata changamoto  gani alipokuwa mtu wa kwanza kufika kwenye kilele cha Mlima Everest?  Akasema changamoto kubwa aliyoipata  ni ya kisaikolojia  ambayo ilikuwa inamsumbua kutoka kuongea  mpaka kuthubutu kwa kusema “Sitaweza” na “Haitawezekana”.  

Hivyo basi changamoto kama hii inawapata wengi kwa kukata tamaa kabla hawajajaribu kufanya kitu.  Muda wote tunaona hatuwezi kwa sababu hatutaki kujaribu.  Sir Edmund  Hillary alifika juu ya kilele cha mlima Everest na akaonyesha inawezekana na baadae ikawa rahisi kwa wengine.   Mwingine nae baada ya kuona imewezekana kwa Sir Hillary nae anasema ngoja nami niupande mlima huu.  Sasa hivi hata  watalii wengi tu wanaupanda  mlima Everest bila hofu yoyote sio mlima mpendwa msomaji  ila ni sisi wenyewe ndio mlima.  

Kila wakati unamaliza jambo hata likiwa dogo, unaongeza na hali yako mwenyewe ya kufanya, pia unapiga  picha yako, pia unaongeza na mawazo yako.  Unaweka  akiba kidogo  ya ujasiri.  Unasema kutokea ndani, “Niko sawa” “niko sawa” angalia navyofanya!!!  Kila utakavyofanya hivyo basi  unaweza kufanya kitu zaidi na zaidi.  Inaanza kidogo kidogo  mpaka unamaliza kufanya jambo kubwa sana!!!  Lakini kumbuka inaanzia kwako, amini mwenyewe na ondoa  adui wa ndani yako ambaye anasema siwezi na yeye akikubali basi kila kitu kinakuwa sawa!!!

Adui wa pili anayeua ndoto yako ni kusumbukia vitu vidogovidogo, au kukaa na watu wanaosema haiwezekani.  Wote wanaotumia neno haiwezekani au siwezi unawajua, hauwezi kufanya haya wewe ni mzee, hauwezi kufanya hivi kwa kuwa hauna elimu ya kutosha, hauwezi kufanya  lazima uwe na sifa hizo kwanza hapa hauna sifa kulingana na kazi yenyewe, hauwezi kufanya kazi hivyo inaonyesha jinsi gani ukate tamaa na kuacha kufikiria makubwa.  Hauwezi!  Hauwezi! Hauwezi!! Acha hiyo hali ya huzuni, unaweza kufanya  kitu chochote  ni kweli kama unataka kufanya.  Kama una ndoto na ukaifuata ndoto yako.  Basi  hakikisha unaifikia hiyo ndoto kama ulivyoota. Usiangalie watu wanasema nini na wanakuonaje kwa nje kama ipo ipo tu lazima itimie!!!!!!!

Na Lusako Mwakiluma

No comments:

Post a Comment