Monday, March 24, 2014

UNAENDELEA KUSUBIRI MELI YAKO IJE NA UINGIE NDANI



 Watu wengi wanaongea kuhusu kusubiria meli yao ije ili waingie ndani. Wametulia na kusubiria muda ufike.  Nakumbuka katika siku zangu wakati naimba pale kwenye ukumbi fulani nilikuwa nasubiria muda ufike ili nipumzike.  Baadae nikasikia watu  wanazungumza  na kusema endelea kuimba, endelea kuimba, endelea kuimba kuna muda utafika na utapumzika tu.  Niliendelea kusubiria mapumziko yangu lakini hayakutokea.  Baadae  nikaanza kujifunza kwamba mafanikio ni  uamuzi wa mtu na sio kitu kinachotokea kwa bahati kwa binadamu yeyote.

Nimejifunza kwamba  njia nzuri ya kukua katika maisha ni kuanza kukua kwako binafsi.  Ninaanza na kipindi cha  mandeleo yangu binafsi na nimeamua kwamba  sitaweza kusubiria mapumziko yaje. Nitakwenda kujiwekea mapumziko yangu mimi mwenyewe.   Nina uamuzi wangu. Sitaendelea kusubiria  meli yangu ije niingie au itabidi niogelea na kuifuata uko iliko. Ninafuraha kwamba nimefanya kwasababu marafiki zangu wengi wameendelea kusimama na kuendelea kusubiria meli yao ifike ili waingie. 

Jonathan Winters alisema, “Nilisubiria mafanikio lakini sikuyaona, nikaamua kwenda bila mafanikio”  Folks alisema, “Mafanikio sio kitu cha kusubiria…. ni kitu ambacho unatakiwa lazima ukikamilishe na ukipate!!! Usisubirie meli yako ije na uingie…. ebu ingia ogelea na uikute hiyo meli ili upande na uendelee na safari yako!!!! Utafurahia sana kufanya hivyo mara utakapojitambua.  Ebu amka na uanze kuogelea uikute meli yako rafiki, ndugu, mpendwa wangu muda haukusubiri wewe.  Ingia ndani ya maji uanze kuogelea uifuate meli yako popote ilipo na uende safari yako.

Na: Lusako Mwakiluma

No comments:

Post a Comment